Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro itaendelea kutumia vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi katika kutangaza vivutio vya utalii kitaifa na kimataiifa ili kuvutia watalii wengi zaidi.

Akitoa mada katika mkutano wa waandishi wa habari vijijini Afisa Uhifadhi Mkuu Uhusiano kwa umma Ngorongoro, Kassim Nyaki amesema vyombo vya habari vina nguvu kubwa katika kufikia watu wengi kwa wakati mmoja hivyo Ngorongoro inatumia Fursa hiyo kuhakikisha kila Mtanzania anafikiwa.

Akitoa Mada katika mkutano huo Afisa Utalii Ngorongoro COII Hillary Kimaro ameeleza kuwa Ngorongoro ni kitovu cha Maajabu mengi (Destination of Many Wonders) ambapo eneo hilo la Urithi wa Dunia linalokusanya wanyamapori, malikale, urithi wa utamaduni pamoja na kushuhudia pumzi ya kwanza ya ndama kuzaliwa kabla ya kuhama kwa nyumbu katika eneo la Ndutu.

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini (RUJAT) Neville Meena ameipongeza Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa kuthamini mchango wa waandishi wa habari katika kutangaza utalii wa nchi yao ili kuendelea kuvuta maelfu ya watalii kutoka kila pembe ya dunia