Mwenyekiti wa ALAT Taifa Sima Costantine akizungumza na waandishi wa habari kuelekea Mkutano mkuu

………

Na Hellen Mtereko, Mwanza

Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya TAWALA za Mitaa Tanzania (ALAT) unatarajiwa kufanyika Jijini Mwanza na utajumuisha Halmashauri 184 pamoja na wajumbe mbalimbali wakiwemo Mameya wa nchi nzima.

Mkutano huo ni moja ya mikutano ya kikanuni na unatarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 500 ambapo utafanyika Novemba 14 hadi 26 mwaka huu Jijini Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa Habari Mwenyekiti wa ALAT Taifa, Sima Costantine amesema mkutano huo utakuwa na sehemu mbili ambapo mkutano wa kwanza utakuwa ni mkutano mkuu ambao utajadili mambo yatokanayo na Halmashauri.

“Mkutano wa pili utakuwa ni wakazi ambao utazikutanisha taasisi mbalimbali zinazofanya kazi na Serikali za mitaa ambapo zitapata nafasi ya kuwasilisha mawasilisho na kutoa ajenda mbalimbali; Amesema Sima

Sima Amesema maandalizi ya mkutano huo tayari yameshaanza kufanyika huku akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwanamna anavyoendelea kuruhusu na kutoa vibali vya kufanyika kwa mkutano huo.

Aidha, ametoa rai kwa wananchi wa Mkoa wa Mwanza kuendelea kuwa wakarimu kwaajili ya kuwapokea wageni kwani ugeni huo ni mkubwa na utakuwa na fursa nzuri hususani katika kukuza uchumi.

Ameeleza kuwa Mkoa wa Mwanza unavivutio mbalimbali ikiwemo Hifadhi ya kisiwa cha Saa nane hivyo wanaendelea kuangalia namna nzuri ili wageni watakapofika waweze kutembelea vivutio hivyo.