NA DENIS MLOWE, IRINGA
MKUU wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, amewataka wananchi kujenga utamaduni wa kuchangia damu kwa hiari ili kusaidia kuokoa maisha ya watu wanaohitaji huduma hiyo katika hospitali mbalimbali.
Wito huo umetutoa, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, kitengo cha damu salama, wakati wa hafla ya uchangiaji damu iliyoandaliwa na Rotary Iringa Club kwa kushirikiana na hospitali hiyo.
Akizungumza katika hafla hiyo akiwa mgeni wa heshima, Kheri amesema damu ni huduma muhimu katika kuokoa maisha ya wagonjwa mbalimbali, wakiwemo kina mama wanaojifungua, watu wanaopata ajali na wagonjwa wengine wanaohitaji kuongezewa damu.
Amesisitiza kuwa damu inayotumika kwa ajili ya matibabu hupatikana kupitia uchangiaji wa binadamu, hivyo ni muhimu kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kuchangia damu ili kuhakikisha wahitaji wanapata huduma hiyo kwa wakati.
Amesema mwitikio wa wananchi katika kuchangia damu ni sehemu muhimu ya juhudi za kuokoa maisha ya watu wanaokabiliwa na changamoto za kiafya zinazohitaji kuongezewa damu.