Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Ellen Maduhu, amekutana na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mhe. Dkt. Bekir Gezer, katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam, tarehe 23 Oktoba 2026.
Mazungumzo hayo yalijikita katika kujadili mipango ya baadaye na matukio ya pamoja yanayolenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano wa pande mbili kati ya Tanzania na Uturuki.
Aidha, viongozi hao walijadili changamoto za kiutendaji na uratibu zinazohitaji kushughulikiwa ili kuwezesha utekelezaji wa mipango hiyo kwa ufanisi. Pia walibadilishana mawazo kuhusu changamoto ambazo bado hazijapatiwa ufumbuzi, kwa lengo la kutafuta njia za kuzitatua na kuendeleza ushirikiano wenye manufaa kwa nchi hizo mbili.

