Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kushirikiana na wananchi na wadau wengine katika kuimarisha ulinzi na usalama wa maisha na mali za wananchi, kwa kuendeleza mikakati ya kubaini na kuzuia uhalifu.
Mnamo Oktoba 16, 2026 saa 11:45 alfajiri huko katika Mtaa wa Makunguru, Kata ya Ruanda, Tarafa ya Iyunga Jijini Mbeya, Nice Kabuje, mhudumu wa nyumba ya kulala wageni iitwayo Igogwe na mkazi wa Makunguru Jijini Mbeya alitoa taarifa Kituo cha Polisi Mbeya Mjini kuwa katika nyumba hiyo ya kulala wageni chumba kilichopewa jina la Uphilipino imekutwa miili ya watu wawili jinsia ya kike wakiwa wamefariki dunia na kufichwa uvunguni mwa kitanda.
Kufuatia taarifa hiyo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifika eneo la tukio na kuanza uchunguzi ambapo mwili mmoja ulitambulika kuwa ni wa Annastazia Mwakipesile (32) aliyekuwa mkazi wa Kabwe na mwili mwingine bado haujatambuliwa mpaka sasa na umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Kanda Mbeya.
Mnamo Oktoba 21, 2026 saa 9 alasiri huko Iyela Jijini Mbeya katika ufuatiliaji wa waliohusika na mauaji hayo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanikiwa kumkamata mtuhumiwa Benson Steven maarufu kwa jina la Mkembo, fundi sofa na mkazi wa Iwambi Jijini Mbeya kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo.
Uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha matukio hayo ni imani za kishirikina kwa lengo la kupata utajiri kwani alieleza kabla ya kufanya kitendo alikwenda kwa mganga. Mtuhumiwa alikubali kwa hiari yake kuwaongoza Askari hadi nyumbani kwa Mganga wa jadi aliyempa masharti hayo ili apate utajiri.
Wakiwa njiani wakielekea kwa Mganga huyo ghafla mtuhumiwa aliruka kutoka kwenye gari na kuanza kukimbia hali iliyopelekea Askari kufyatua risasi tatu juu kwa lengo la kumtahadharisha na kumtaka asimame lakini aliendelea kukimbia ndipo Askari alifyatua risasi iliyompata kwenye paja la mguu wa kushoto.
Mtuhumiwa alikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa Kanda Mbeya kwa matibabu kutokana na jeraha alilolipata lakini alifariki dunia akiwa anaendelea kupatiwa matibabu.
Aidha, kumbukumbu zinaonyesha kuwa mtuhumiwa Benson Steven maarufu kwa jina la Mkembo aliwahi kukamatwa Temeke Dar es Salaam na kushtakiwa kwa kosa la kuvunja nyumba usiku na kuiba ambapo alitiwa hatiani na kufungwa jela mwaka mmoja na baada ya kumaliza kifungo alikuja Mbeya.
Pia zinaonyesha mnamo Desemba 29, 2025 huko Iwambi Mbeya alikamatwa akiwa na wenzake 8 na kufikishwa Mahakamani kwa kesi ya Unyang’anyi wa kutumia Silaha ambapo waliachiliwa huru baada ya mlalamikaji kuugua na kushindwa kufika Mahakamani kutoa ushahidi.
KATAZO LA BAJAJI KUPITA BARABARA KUU NA KUFUATA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI.
Itakumbukwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Jumanne Sagini mnamo Oktoba 12, 2026 alifanya kikao na wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo Maafisa Usafirishaji wa Mkoa wa Mbeya na kutoa maelekezo kwa Jeshi la Polisi kuhusu katazo la Bajaji kupita barabara kuu ya TANZAM (Tanzania – Zambia) na badala yake kutumia barabara za mitaa na kuhakikisha Bajaji zote zinafuata sheria za usalama barabarani.
Katika kuendelea kutekeleza jukumu hilo, Oktoba 19, 2026 saa 8 mchana Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilianza kusimamia utekelezaji wa maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwa kufanya misako na doria ili kuwakamata Madereva wote waliokuwa wanakiuka sheria za usalama barabarani na kufanya fujo ambapo jumla ya Madereva 19 pamoja na Bajaji 19 zilikamatwa na kufikishwa Kituo cha Polisi Mwanjelwa kwa hatua zaidi za kisheria.
Madereva 18 kati yao walifikishwa Mahakama ya Mwanzo Mbeya mjini Oktoba 20, 2026 na kushtakiwa kwa kosa la kufanya fujo ambapo walitiwa hatiani na kufungwa jela mwezi mmoja. Vile vile watuhumiwa wengine 8 walifikishwa Mahakamani kwa kosa la kuharibu mali ambapo walivunja vioo vya mabasi/daladala 11 na kesi yao inaendelea kusikilizwa Mahakamani hapo.
Hata hivyo vurugu hizo ziliendelea ambapo Oktoba 20, 2026 makundi madogo madogo ya vijana yaliendelea kufanya fujo na kufunga barabara za mitaa ya Nanenane na katika fujo hizo vijana 5 walikamatwa na Oktoba 21, 2026 walifikishwa Mahakama ya Mwanzo Mbeya mjini na Mshitakiwa mmoja alipatikana na hatia baada ya kukiri kosa na kufungwa jela mwezi moja huku washitakiwa wengine 4 kesi yao inaendelea kusikilizwa Mahakamani hapo.
Katika muendelezo wa mgomo huo, Oktoba 21, 2026 saa 9 alasiri Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Mhe Patrick Mwalunenge alifanya mkutano na Maafisa Usafirishaji hao ambao walianza maandamano yasiyo halali kuelekea Gereza la Ruanda na Kituo cha Polisi Mbeya kutaka kwenda kuwatoa wenzao waliokamatwa na kufungwa ndipo Jeshi la Polisi liliwatawanya na kuwakamata wagomaji na waandama
