Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga SC, wameandika historia kwa kutinga hatua ya makundi ya mashindano ya klabu barani Afrika kwa mara ya tano mfululizo, baada ya kuisambaratisha CFFA ya Madagascar kwa jumla ya mabao 8-1 katika msimu wa 2026/2027.
Matokeo hayo yamepatikana leo, Oktoba 21, 2026, baada ya Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 katika mchezo pili uliopigwa katika Uwanja wa Jamhuri, Dar es Salaam na kufanikiwa kukata tiketi ya hatua ya makundi kwa kishindo, ambapo mchezo kwanza Yanga waibuka na ushindi wa mabao 4-0.
Safari ya mafanikio hayo ilianza msimu wa 2022/2023, wakati Yanga ilipotinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika na baadaye kufanikiwa kucheza fainali ya mashindano hayo.
Msimu uliofuata wa 2023/2024, Yanga ilishiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na kufanikiwa tena kutinga hatua ya makundi, kabla ya kusonga hadi robo fainali, ambako ilitolewa na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kwa mikwaju ya penalti 4-2 baada ya sare ya jumla.
Katika msimu wa 2024/2025, kikosi hicho, kilichokuwa chini ya kocha Miguel Gamondi, kiliendeleza mwenendo huo kwa kufanikiwa tena kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Msimu uliopita wa 2025/2026, Yanga iliendelea kushiriki hatua hiyo, na sasa imekamilisha safari ya kufuzu kwa mara ya tano mfululizo msimu huu wa 2026/2027.
Ushindi wa jumla wa mabao 8-1 dhidi ya CFFA unaendeleza rekodi ya Yanga katika mashindano ya klabu barani Afrika na kuipa nafasi ya kuendelea kuwakilisha Tanzania katika hatua ya makundi ya msimu huu.
