Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inatoa taarifa ya uwepo wa mgandamizo mdogo wa hewa katika Bahari ya Hindi karibu na Visiwa vya Ushelisheli katika umbali wa takribani kilomita 1600 kutoka pwani ya nchi yetu.

Uchambuzi wa mifumo ya hali ya hewa unaonesha kuwa mgandamizo huo mdogo wa hewa unatarajiwa kuimarika na kuwa Kimbunga katika eneo hilo la Bahari ndani ya kipindi cha siku nne zijazo na mgandamizo huo unaelekea pwani ya nchi yetu. Aidha, uwepo wake katika Bahari ya Hindi unatarajiwa kuimarisha kiasi mifumo inayosababisha mvua katika maeneo ya ukanda wa pwani ya nchi yetu na maeneo jirani hususani kuanzia tarehe 24 Oktoba, 2026.

USHAURI: Watumiaji wa bahari na jamii kwa ujumla wanashauriwa kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania pamoja na kupata ushauri na miongozo ya wataalam wa kisekta.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kufuatilia mwenendo wa mgandamizo huo mdogo wa hewa pamoja na athari zake kwa mifumo ya hali ya hewa hapa nchini na itaendelea kutoa taarifa kila inapobidi.