Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya SACP Benjamin Kuzaga, leo Oktoba 14, 2026 amefika Kata ya Ilemi Jijini Mbeya na kuonana na Mtendaji wa Kata hiyo, Wenyeviti wa Mitaa na baadhi ya Wananchi na kuzungumzia hali ya ulinzi na usalama.

Ziara hiyo ni kufuatia kusambazwa kwa taarifa katika moja ya mitandao ya kijamii ikisema kumekuwepo na ongezeko la matukio mengi ya uhalifu katika Mitaa ya Kata ya Ilemi.

Viongozi na baadhi ya wananchi wa Kata hiyo wamefunguka na kueleza mikakati na jitihada zinazofanywa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kupitia Polisi Kata kwa kushirikiana na Viongozi na Wananchi waliopo katika Mitaa ya Kata hiyo hali inayopelekea kuwepo kwa amani na utulivu.