Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Smita Bhalia akimuonesha moja ya mfumo unaotumiwa na Taasisi hiyo kutafsiri lugha mbalimbali Kansela wa Uchumi na Biashara kutoka ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania Chu Kun alipotembelea tawi la JKCI Oyster bay kwaajili ya kujione huduma za kibingwa za magonjwa ya moyo zinazotolewa na taasisi hiyo.
Kansela wa Uchumi na Biashara kutoka ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania Chu Kun akizungumza na Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Smita Bhalia alipotembelea tawi la JKCI Oyster bay kwaajili ya kujionea huduma za kibingwa za magonjwa ya moyo zinazotolewa na taasisi hiyo.
Kansela wa Uchumi na Biashara kutoka ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania Chu Kun akiangali dawa zilizopo katika duka la dawa la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) tawi la Oyster Bay alipotembelea tawi hilo kwaajili ya kujionea huduma za kibingwa za magonjwa ya moyo zinazotolewa na taasisi hiyo.
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Smita Bhalia, Kansela wa Uchumi na Biashara kutoka ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania Chu Kun na baadhi ya wafanyakazi wa JKCI wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ziara fupi iliyofanywa na kansela huyo katika tawi la JKCI Oyster bay kwaajili ya kujione huduma za kibingwa za magonjwa ya moyo zinazotolewa na taasisi hiyo.
Picha na JKCI
……………
Na. Mwandishi Maalum – Dar es Salaam
11/10/2026 Kansela wa Uchumi na Biashara kutoka ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania Chu Kun amevutiwa na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) katika tawi lake la Oyster bay lililopo jijini Dar es Salaam.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya kansela huyo kufanya ziara katika Kliniki ya JKCI Oyster bay na kupata fursa ya kujionea namna ambavyo huduma zinatolewa pamoja na uwekezaji wa vifaa tiba vya kisasa vilivyowekezwa katika tawi hilo.
“Nimefurahishwa na uwekezaji mkubwa uliofanyika katika taasisi hii hususan uwepo wa vifaa tiba vya kisasa na ubora wa huduma zinazotolewa kwa wananchi”, alisema Chu Kun
Tawi la JKCI lililopo Oyster bay ni sehemu ya juhudi za Taasisi hiyo za kusogeza huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo karibu na wananchi kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa huduma bora na kupanua wigo wa huduma za kibingwa nchini.
