Watendaji wa Sekta ya Maji wametakiwa kusimamia miradi inayotekelezwa iendane na thamani ya fedha.

Naibu Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Kundo Andrea Mathew (Mb) amesema hayo katika kikao kazi na watendaji wa sekta ya maji Mkoa wa Tabora leo Jumapili tarehe 11 Oktoba, 2026.

Mhe. Kundo amepokea taarifa kuhusu miradi mbalimbali ya maji inayotekelezwa, hatua iliyofikiwa, changamoto na mikakati iliyowekwa ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma.

Mhe. Kundo amewataka watendaji wa sekta ya maji kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi, na kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa kuzingatia viwango na ubora. 

Amesisitiza umuhimu wa watendaji kuwajibika katika kutatua changamoto za huduma ya maji na kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa uhakika na endelevu.