Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.
Mazungumzo hayo yamefanyika katika muktadha wa majukumu ya Dkt. Kikwete kama Mwakilishi wa Ngazi ya Juu wa Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika kuhusu Pembe ya Afrika na Bahari ya Shamu, pamoja na juhudi za kuendeleza amani nchini Sudan Kusini.
Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Togolani Mavura.
