Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Majadiliano na Utatuzi wa Migogoro Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. Benno Anthony Sanga ameiwakilisha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati wa ufunguzi rasmi wa Kongamano na Wiki ya Utatuzi wa Migogoro ya Kibiashara tarehe 1 Oktoba, 2026 Jijini Dar es Salaam.
Kongamano hilo limefunguliwa rasmi na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Alice E. Mturo aliyemuwakilisha Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, *Mhe. Zainab Athuman Katimba.
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ni miongoni mwa Wadhamini wa Kongamano na Wiki ya Utatuzi wa Migogoro ya Kibiashara Tanzania 2026 inayoratibiwa na Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi Tanzania (TIAC) na kubeba kauli mbiu isemayo *“Kujenga Imani katika Utatuzi wa Migogoro kwa Njia Mbadala (ADR): Kuimarisha Ufanisi, Upatikanaji na Ubunifu katika Utatuzi wa Migogoro ya Kibiashara”.

