Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi (kushoto) akimkabidhi nyaraka za ofisi Jubilate Lauwo (kulia) ambae ameteuliwa kuwa mkuu wa Wilaya hiyo

Na Hellen Mtereko,Mwaza

Aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Jubilate Lauwo ameomba ushirikiano kwa watumishi wa wilaya hiyo ili waweze kufanya kazi ya kuwahudumia wananchi vizuri.

Ombi hilo amelitoa Leo Oktoba 01, 2026 wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Amina Makilagi ambae amehamishiwa Wilaya ya Magu.

Amesema endapo watashirikiana kwa pamoja wataweza kufanya kazi kwa uaminifu,weledi na uadilifu hususani katika kutatua changamoto za wananchi.

Amesema Nyamagana inawatu ambao wanajishughulisha na shughuli mbalimbali za uzalishaji hivyo inahitaji amani,utulivu na usalama wa hali ya juu.

“Nitashirikiana vema na kamati ya usalama ili wananchi wetu wazidi kufanya shughuli zao za uzalishaji vizuri”,

Aidha, amesema kuwa kauli mbiu yake ya utendaji kazi katika wilaya hiyo itakuwa ni ‘Tushirikiane tusikilize wananchi tulinde amani ya Nyamagana tuweke maendeleo ya wananyamagana mbele’

Kwaupande wake Msitahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Constantine amesema anaimani kubwa na Mkuu wa wilaya kutokana na utendaji kazi wake, hivyo ameahidi kumpa ushirikiano ili wazidi kupiga hatua zaidi katika kuwaletea wananchi maendeleo