Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Helman Nicholaus akimpima shinikizo la damu abiria aliyesafiri na treni ya SGR wakati wa kambi maalumu ya siku saba iliyokuwa ikifanywa na watalamu wa JKCI kwakushirikiana na Shirika la Reli Tanzania (TRC) katika kuadhimisha siku ya moyo duniani. Jumla ya abiria 1,420 wamefanyiwa uchunguzi wa afya.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Agnes Lugendo akimuuliza maswali ya ufahamu wa magonjwa ya moyo abiria aliyesafiri na treni ya SGR wakati wa kambi maalumu ya siku saba iliyokuwa ikifanywa na watalamu wa JKCI kwakushirikiana na Shirika la Reli Tanzania (TRC) katika kuadhimisha siku ya moyo duniani. Jumla ya abiria 1,420 wamefanyiwa uchunguzi wa afya.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Yvonne Mushi akiangalia uzito wa abiria aliyesafiri na treni ya SGR wakati wa kambi maalumu ya siku saba iliyokuwa ikifanywa na watalamu wa JKCI kwakushirikiana na Shirika la Reli Tanzania (TRC) katika kuadhimisha siku ya moyo duniani. Jumla ya abiria 1,420 wamefanyiwa uchunguzi wa afya.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Salma Jamaldin akimpima shinikizo la damu abiria aliyesafiri na treni ya SGR wakati wa kambi maalumu ya siku saba iliyokuwa ikifanywa na watalamu wa JKCI kwakushirikiana na Shirika la Reli Tanzania (TRC) katika kuadhimisha siku ya moyo duniani. Jumla ya abiria 1,420 wamefanyiwa uchunguzi wa afya.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Nancy Mallya akimuuliza maswali ya ufahamu wa magonjwa ya moyo abiria aliyesafiri na treni ya SGR wakati wa kambi maalumu ya siku saba iliyokuwa ikifanywa na watalamu wa JKCI kwakushirikiana na Shirika la Reli Tanzania (TRC) katika kuadhimisha siku ya moyo duniani. Jumla ya abiria 1,420 wamefanyiwa uchunguzi wa afya.
………….

Abiria 1,420 waliosafiri na treni ya mwendokasi (SGR) wamefanyiwa uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya moyo duniani ambayo hufanyika kila ifikapo tarehe 29 mwezi Septemba.
Matibabu hayo yaliyomalizika jana yamefanyika katika kambi maalum ya siku saba iliyokuwa ikifanywa na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Shirika la Reli Tanzania (TRC).

Akizungumza wakati wa kuhitimisha kambi hiyo Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Samweli George alisema abiria 649 walifanyiwa kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO) na abiria 773 walifanyiwa kipimo cha kuangalia mfumo wa umeme wa moyo (Electrocardiography – ECG).

“Baada ya kuwafanyia uchunguzi wa afya abiria hao, abiria 165 tuliwakuta na changamoto mbalimbali za afya ambazo zilihitaji uchunguzi zaidi hivyo kuwapa rufaa kufika katika Taasisi yetu kwaajili ya kuchunguzwa na kupewa matibabu zaidi”, alisema Dkt. Samweli.

Dkt. Samweli alisema kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara ni muhimu kwani humsaidia mtu kujitambua na kuchukua hatua za mapema pale anapokutwa na changamoto za afya kabla ya changamoto zile hazijamsababishia madhara makubwa.

Wakiongea kwa nyakati tofauti wananchi waliopatiwa huduma katika kambi hiyo wameishukuru Serikali ya awamu ya sita na kuomba huduma hizo kuendelea kutolewa katika usafiri wa treni ya mwendokasi (SGR).

Grace Donald alisema usafiri wa mwendo kasi umetulia, hauna changamoto za kurushwa hivyo kutolewa huduma za uchunguzi na matibabu wakati wa safari kunarahisisha upatikanaji wa huduma za afya na ni rahisi kwa abiria kutembea na kuzifuata zinapotolewa.

“Haikuwa ngumu kwetu abiria kutembea kuzifuata huduma za matibabu ya moyo katika behewa lililokuwa linatoa huduma kutokana na utulivu wa usafiri wa SGR, ni muhimu sasa tukarahisishiwa hivi matibabu hata kama ni kwa kulipia ili hata ukikosa muda wa kwenda hospitali wakati uko kwenye safari zako unapima afya”, alisema Grace