Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) ni miongoni mwa taasisi kumi za Serikali nchini zilizooongoza katika ufanisi wa mapato, matumizi bora ya fedha za umma kwa tija na umahiri katika rejesho la mtaji kwa mashirika ambayo ni ya kibiashara.
Akielezea kuhusiana na taasisi hizo kumi zilizotajwa vinara katika kundi hilo Msajili wa Hazina Bw. Nehemia Mchechu amesema mashirika yaliyofanya vizuri katika kundi hilo yameonesha umahiri mkubwa katika kudhibiti matumizi, kuongeza mapato na kusimamia vema rejesho Serikalini sambamba na utoaji huduma kidijitali kwenye utoaji wa huduma kwa wateja.
Kikao hicho kilichofunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi kimehudhuriwa pia na Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi NCAA Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Venance Mabeyo Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka hiyo Abdul-Razaq Badru ,Ngorongoro imeonesha ushiriki wake kwa kutangaza vivutio vya utalii mubashara kupitia luninga kubwa iliyopo nje ya ukumbi wa mikutano AICC jijini Arusha.
Katika kipindi cha miaka ya hivi Karibuni NCAA imejipambanua katika kujitangaza kimkakati pamoja na kuibua vivutio vya mazao mapya ya utalii katika kampeni inayojulikana kama Ngorongoro Beyond the Crater.
Katika ufunguzi wa kikao hicho Mheshimiwa makamu wa Rais aliwataka viongozi wa mashirika ya umma na binafsi kuja na mpango mkakati wa kutoa mafunzo kwa vitendo na kujitolea (intenship) kwa vijana 10,000 kila mwaka.

