Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dennis Londo (Mb.), amewasili jijini Muscat, Oman, Septemba 27, 2026, kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Uwili baina ya Tanzania na Oman unaotarajiwa kufanyika Septemba 28, 2026.
Mkutano huo unalenga kuimarisha uhusiano wa kimaendeleo na kiuchumi baina ya Tanzania na Oman, pamoja na kujadili maeneo ya kimkakati ya ushirikiano ikiwemo Siasa, uwekezaji, biashara, Madini, nishati na uchumi wa buluu.
Maeneo mengine yatakayojadiliwa ni pamoja na miundombinu na usafirishaji, Elimu, Maji, kilimo, mifugo, utalii na malikale, yanayogusa pia uhusiano wa kihistoria na kitamaduni unaozihusisha Tanzania na Oman.
Makubaliano yatakayofikiwa katika mkutano huo yanatarajiwa kuweka msingi wa kukuza na kuendeleza ushirikiano Katika Sekta hizo kwa manufaa ya pande zote mbili.

