Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dennis Londo (Mb.), amewasili jijini Muscat, Oman kushiriki Mkutano wa Kwanza wa Mashauriano ya Kisiasa baina ya Tanzania na Oman unaotarajiwa Kufanyika, Septemba 28, 2026.
Mkutano huu wa kihistoria, ambao ni wa kwanza tangu kusainiwa kwa Mkataba wa Mashauriano ya Kisiasa mwaka 2009, unafanya tathmini ya jumla ya ushirikiano wa kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Pande zote mbili zitajadili sekta za kimkakati ikiwemo biashara, uwekezaji, madini, nishati, uchumi wa buluu, miundombinu, kilimo, elimu, utalii, urithi, utamaduni na michezo.
Mashauriano haya yanaweka msingi kuelekea Mkutano wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) utakaofanyika Novemba 2026, nchini Tanzania.

