Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara, Ndugu Aggrey Mwanri, amewataka viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuanzia ngazi ya shina, kata, wenyeviti wa mitaa, madiwani na wabunge kutoa elimu kwa wananchi kuhusu tahadhari na madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na mvua za El Niño.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara wilayani Rombo, Mwanri amesisitiza kuwa viongozi hao wanapaswa kuhakikisha suala la athari za mvua hizo linakuwa ajenda katika vikao vyao, ili kuwezesha wananchi kujiandaa mapema na kuchukua hatua za kujikinga na madhara yanayoweza kutokea.

Mwanri amesema chama tawala kinapaswa kuwa karibu na wananchi, kutambua changamoto zao na kushirikiana nao katika kutafuta suluhisho.

“Chama tawala ni kile kinachowajali wananchi wake na kujua namna ya kutatua changamoto zao,” amesema Mwanri.