Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi akisalimiana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Mhe. Antonio Guterres, kabla ya mazungumzo yao yaliyofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa – New York nchini Marekani. Mazungumzo hayo yamefanyika wakati Makamu wa Rais alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 18 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA 81) uliyofanyika New York.