Kamati ya Ushauri wa Kisheria Mkoa wa Mwanza imekutana na kufanya kikao chake cha kwanza katika Mwaka wa Fedha 2026/27, kikao hicho kimefanyika tarehe 26 Septemba, 2026.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya Kisheria ya Mkoa wa Mwanza, ambaye ni Wakili wa Serikali wa Mkoa wa Mwanza, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, *Bw. Kabyemela S. Lushagara,* ameiongoza Kamati hiyo kutoa huduma ya ushauri wa kisheria bila malipo kwa Wananchi wa Mkoa wa Mwanza
Aidha, Kamati hiyo ina jukumu la kufanya uchambuzi na kutoa ushauri wa kisheria kutokana na malalamiko yanayowasilishwa na wananchi ili kupata ufumbuzi na kuwezesha upatikanaji wa haki kwa wananchi.
Katika hatua nyingine, Kamati hiyo imesikiliza na kuyatafutia ufumbuzi malalamiko ishirini na nne (24) yaliyowasilishwan mbele ya Kamati.

