Na Mwandishi wetu, Geita
WAKALA wa vipimo (WMA) wameshiriki maonyesho ya kitaifa ya tisa ya teknolojia ya madini yanayofanyika mjini Geita kwa kuitaka jamii kutembelea banda lao ili kupatiwa elimu juu ya vipimo.
Meneja wa wakala wa vipimo Mwanza Karim Zuberi akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya kitaifa ya teknolojia ya madini Manispaa ya Geita amesema WMA inawakaribisha wadau wote.
Zuberi wadau wote wa maendeleo na wananchi kwa ujumla wanakaribishwa kutembelea banda lao ili kupata elimu juu ya wakala wa vipimo na wanaruhusiwa kuuliza maswali.
Amesema kwenye maonyesho hayo ya teknolojia ya madini wakala wa vipimo ina hakiki mizani zinazotumika kununua madini na vito vya thamani na migodini.
“Katika masoko ya kuuzia madini na kwa wauzaji wa madini (sonara) pia tunatoa ushauri wa kitaalamu kwa Wizara inayohusika na madini mara kwa mara panapohitajika,” amesema.
Amesema wakala wa madini inafanya uhakiki wa vipimo katika maeneo mbalimbali ya biashara kama maduka ya kuuzia nyama, viwandani, mizani inayotumia kuuzia bidhaa masokoni ikiwemo bidhaa zinazofungashwa.
“Wakala wa vipimo hufanya hivyo ili kuhakikisha wananchi wanapata bidhaa kwa usahihi kulingana na thamani ya fedha inayotolewa na siyo vinginevyo,” amesema.
Amesema kwamba kwenye sekta ya maji wakala wa vipimo inafanya uhakiki wa mizani zote zinazotumika wakati wa ununuzi wa mazao mbalimbali kama vile pamba, korosho na ufuta.
Ameeleza kuwa uhakiki huo wa mizani ya vyama vya msingi vya ushirika na makampuni yanayonunua mazao hufanyika kwa msimu kuanza na usimamizi mara baada ya msimu kuanza ili kujiridhisha kama inatumika kwa usahihi.
Hata hivyo amewakaribisha wakati wa Geita na wananchi wote wanaoshiriki kwenye maonyesho ya kitaifa ya teknolojia ya madini kupita katika banda lao la wakala wa vipimo ili kupata elimu zaidi juu ya vipimo.
