Na Sixmund Begashe, Moshi
TIMU za Maliasili Sports Club za mchezo wa Kamba ya Wanaume (ME), pamoja na Kamba Wanawake (KE) zimetinga 16 bora kwenye michuano ya SHIMIWI 2026, Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Akizindua rasmi michuano hiyo ya SHIMIWI 2026 kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Paul Makonda, amezipongeza Club zote zinazoshiriki michezo hiyo kwa kuwa mbali ya kupambania ushindi, michuano hiyo ni sehemu muhimu ya kudumisha amani na mshikamano wa Kitaifa.
Mhe Makonda amewaahidi kuwa, mwaka 2027 michuano hiyo itakapofanyika Mkoani Arusha atachangia Sh milioni 500 ili zitumike kama zawadi kwa washindi mbalimbali jambo lililopokewa kwa shangwe kubwa na wanamichezo wote.
Pamoja na viongozi wengine, uzinduzi wa michuano hiyo umeshuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bw. Bernard Marcelline.

