NEW YORK, Marekani | Septemba 2026

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ameshiriki kikao cha Baraza la Kutokomeza Malaria Duniani (End Malaria Council) jijini New York, Marekani.

Kikao hicho kimewakutanisha viongozi na wadau mashuhuri duniani katika kuendeleza juhudi za kutokomeza malaria, wakiwemo Bill Gates, Mwanzilishi Mwenza wa Microsoft na Mkurugenzi wa Gates Foundation; Ray Chambers, Balozi wa Baraza la Afya Duniani, Rais Mstaafu Ellen Johnson Sirleaf; Dkt. H. Fisk Johnson, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wa SC Johnson na viongozi wengine wa kimataifa.

Ushiriki wa Dkt. Kikwete unaendelea kuakisi dhamira yake katika kuimarisha juhudi za kimataifa za kuhakikisha dunia inafikia lengo la kuwa huru dhidi ya malaria.