Na Mwandishi wetu, Geita
KAMPUNI ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya TG Goodness Group, Nyamitondo Geita wameshiriki maonyesho ya tisa ya kitaifa ya teknolojia ya madini yanayofanyika viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan manispaa ya Geita.
Katibu Mkuu wa mgodi huo John Jande Richard amesema baadhi ya wachimbaji wa mgodi huo wamefika kwenye maonyesho hayo na kushiriki mafunzo kwa wachimbaji wadogo yaliyotolewa na Osha.
Jande amesema pamoja na kuwa ni mara yao ya kwanza kwa wafanyakazi wa mgodi wao kushiriki maonyesho hayo ila wamenifaika kupitia elimu ya usalama migodini waliyopatiwa na Wakala wa usalama na afya mahali pa kazi (OSHA).
Amesema wamenufaika na nasaha za Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi , Ajira na Mahusiano Deus Sanga alipofungua mafunzo hayo ya wachimbaji madini.
“Maonyesho ni mazuri wachimbaji wengi wameshiriki na tumepata elimu ya uchimbaji madini kwa usalama kupitia kauli mbiu ya Tuamini kazi yako jikinge na ajali,” amesema Jande.
