Timu ya kuvuta kamba ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (NJE Sports).l ushindani mkali dhidi ya Wizara ya Kazi katika mchezo uliopigwa kwenye viwanja vya CCP, Moshi mkoani Kilimanjaro.

Katika mvuto wa kwanza, pande hizo mbili zilioneshana ubabe na nguvu huku kila timu ikipambana kutawala mchezo, hali iliyofanya mvuto huo kumalizika kwa sare baada ya hakuna upande uliofanikiwa kupata ushindi.

Mvuto wa pili ulianza kwa kasi na ushindani mkubwa zaidi, NJE Sports ikijitahidi kutafuta matokeo ya ushindi. Hata hivyo, Wizara ya Kazi ilifanikiwa kutumia vyema nguvu na mbinu zake na kupata ushindi katika mvuto huo.

Licha ya matokeo hayo, NJE Sports imeonesha kiwango kizuri cha ushindani, mshikamano na moyo wa kupambana hadi mwisho, huku ikitarajiwa kurekebisha maeneo yaliyojitokeza kuelekea michezo inayofuata ya mashindano.