Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Viongozi kuhusu afya ya Mama na Mtoto ulioandaliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Africa CDC) uliofanyika pembezoni mwa Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA81) New York nchini Marekani.

Mkutano huo, umehudhuriwa na Viongozi kutoka nchi mbalimbali za Afrika, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, Dkt. Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Africa CDC) Dkt. Jean Kaseya, Mwenza wa Rais wa Benin Bi. Nathalie Vilette Wadagni, Wadau wa Maendeleo wakiwemo, Gates Foundation, Global Fund, Gavi, UNFPA, Unicef, Suzan Thompson Buffett Foundation, Beginning Fund pamoja na Viongozi kutoka Umoja wa Afrika (AU).