Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Ndugu Aggrey Mwanri, amewataka viongozi wa chama kuwa na utamaduni wa kufanya ziara kwa wananchi mara baada ya uchaguzi, kwa lengo la kuwashukuru kwa ushirikiano na imani waliyoonyesha.

Mwanri ameyasema hayo leo, Septemba 24, 2026, wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Makanya, Kata ya Makanya, Wilaya ya Same, Jimbo la Same Magharibi, Mkoa wa Kilimanjaro.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano baina ya viongozi na wananchi katika kutambua na kutatua kero mbalimbali za kijamii, akieleza kuwa ushirikiano huo ni muhimu katika kuhakikisha changamoto zinazowakabili wananchi zinapatiwa majibu kwa wakati.

Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa CCM pamoja na wananchi na wanachama waliojitokeza kushiriki katika shughuli hiyo.