UYUI

Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026 umezindua Boksi Kalavati la Kasisi A lililopo katika barabara ya Ilolangulu–Kasisi A kata ya Ilolangulu wilaya ya Uyui mkoa wa Tabora.

Mradi huo umetekelezwa na serikali kupitia TARURA kwa gharama ya shilingi milioni 102.38 fedha kutoka Tozo ya Mafuta kwa lengo la kutatua changamoto ya muda mrefu ya kujaa maji katika eneo hilo na kuboresha mawasiliano kati ya maeneo yanayounganishwa na barabara hiyo.

Mradi umekamilika kwa asilimia 100 ukihusisha ujenzi wa daraja la zege, uboreshaji wa tuta la barabara, uchongaji wa barabara na uwekaji wa changarawe.

Kukamilika kwa mradi huo kumeondoa kero ya kujaa maji katika eneo hilo, kuimarisha mawasiliano na usafiri, kurahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii na kiuchumi pamoja na kuchochea shughuli za maendeleo kwa wananchi wanaotumia barabara hiyo.

TARURA inaendelea kusimamia na kutekeleza miradi ya miundombinu yenye lengo la kutatua changamoto za wananchi na kuboresha huduma za usafiri na usafirishaji.