Katika picha ni Mkufunzi kutoka chuo cha VETA Dakawa Hamidu Shabani akitoa maelezo kuhusu fursa za mafunzo ya ufundi stadi na kutoa vipepeushi kwa wananchi waliotembelea banda la VETA lilipo katika viwanja vya Dkt Samia Suluhu Hassan kata ya Bombambili Manispaa ya Geita leo tarehe 23 Septemba 2026.
VETA inashiriki katika Maonesho ya Tisa ya Teknolojia ya Madini kwa lengo la kutangaza mafunzo yanayo husiana na Sekta ya madini na fursa za kujiunga katika vyuo vyake sambamba na kuonesha bunifu na teknolojia zilizobuniwa na Wakufunzi na Wanafunzi wa VETA kwaajili ya kutatua changamoto zinazohusiana na Uchumi wa kanda ya Ziwa.
Maonesho hayo yamenza leo na yanatarajiwa kufunguliwa rasmi tarehe 25 Septemba, 2026

