Na Sixmund Begashe, Moshi

TIMU za Maliasili Sports Club Kamba Wanaume (ME) na Wanawake (KE) zinazoshiriki michuano ya SHIMIWI 2026 chini ya mwamvuli wa Wizara ya Maliasili na Utalii, zimeanza kwa kishindo michuano hiyo baada ya timu hizo kushinda mapambano yote kwa ushindi wa 2-0 kila moja. 

Katika mchezo wa awali Kamba ME, timu ya RAS Tabora iliingia mitini na kuikabidhi ushindi usio na jasho wa 2-0 timu ya Maliasili, huku timu ya Maliasili Sports Club Kamba KE, ikichukuwa ushindi mnono wa 2 – O ndani ya sekunde chache kwa kuiburuza timu ya Uwekezaji Kamba KE.

Nayo timu ya Maliasili Sports Club Mpira wa Pete KE inatarajia kuikabili vilivyo timu ya Haki, katika mchezo utakaochezwa hivi karibuni katika viwanja vya Chuo cha Ushirika Moshi.