Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka akiwa ameambatana na Kamati ya Usalama Wilaya, kusikiliza kero za wananchi katika Tarafa ya Mikumi wakati wa ziara yake ya kutatua migogoro, kukagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Kijiji cha Nyamfisi na kufanya mikutano ya hadhara ya kuhamasisha wananchi kushiriki shughuli za maendeleo katika Kata za Vidunda, Ruhembe, Kidodi na Ruaha.