Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amekutana na Waziri wa Afya wa Tunisia Mustapha Farhan ambapo wamejadili kwa kina uwezo wa kuzalisha wa dawa ndani ya nchi, tiba ya mionzi na tiba kwa njia wa mtandao.

Dkt. Mwigulu amesema kuwa katika hali ambapo mnyororo wa ugavi unakatika, ni muhimu kuwa na vyanzo vya bidhaa vilivyotengenezwa ndani ya nchi. “Tunaikaribisha Tunisia kushirikiana na Tanzania katika kuimarisha sekta ya uzalishaji wa dawa.”

Amesema kuwa Tanzania inaona uzalishaji wa dawa ndani ya nchi ni kipaumbele katika kuhakikisha usalama wa afya ya jamii na fursa muhimu ya kuendeleza sekta ya viwanda.

“Wakati wa misukosuko mikubwa ya kidunia kama COVID-19, tuliona wazi umuhimu wa kuimarisha uzalishaji wa ndani wa bidhaa muhimu zikiwemo dawa.”

Dkt. Mwigulu yupo Rome, nchini Italia akimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano wa Kimataifa wa Kujadili Afya Moja na Mifumo ya Chakula na Kilimo, unaofanyika makao makuu ya Shirika la Chakula Duniani (FAO)