Na Sixmund Begashe, Moshi

WANAMICHEZO wa Club za Wizara na Idara zinazoshiriki michezo ya SHIMIWI 2026 Mkoani Kilimanjaro, pamoja na mambo mengine, wametakiwa kutumia fursa hiyo ya michezo kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo Mkoani humo kama itakavyoainishwa kwenye ratiba. 

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) Daniel Mwalusamba, kwenye kikao maalumu kilichojumuisha viongozi wa Club hizo na wanamichezo waliowasili Wilayani Moshi tayari kwa michuano hiyo. 

Bw. Mwalusamba amesema Mkoa wa Kilimanjaro umejaliwa kwa urithi adhimu wa vivutio vya utalii na ndiyo maana nafasi imetengwa kwa wanamichezo hao kutembelea vivutio hivyo wanapaswa kuitumia vizuri nafasi hiyo.

Amewasisitiza wanamichezo hao kutumia michezo hiyo katika kuimarisha udugu, upendo na mshikamano kwa maslahi mapana ya taifa kwa ujumla.

Amewataka viongozi wa Club hizo kusimamia taratibu zote za kiutumishi na kuimarisha mshikamo na udugu miongoni mwa wanamichezo. 

Katika hatua nyingine, wanamichezo wa Club ya Michezo ya Wizara ya Maliasili na Utalii, wameendelea na mazoezi yao ili kujiimarisha zaidi katika michezo iliyo mbele yao.