Na Mwandishi wetu, Babati
SHULE ya awali na msingi ya Tarangire (Tarangire Pre & Primary English Medium School) iliyopo mjini Babati
Mkoani Manyara imeufanya mji wa Babati na viunga vyake kusimama kwa muda wakati wakiadhimisha mahafali ya nane ya darasa la saba mwaka 2026.
Mahafali hayi yamefanyika katika bustani za shule hiyo iliopo mtaa wa Wang’waray Kata ya Babati kilomita tano toka katikati ya mji wa Babati kuelekea barabara ya lango jipya la Mamire la Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.
Shule hiyo ipo karibu kabisa na Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Kampasi ya Babati.
Mgeni rasmi katika mahafali hiyo alikuwa Afisa Elimu ya Sekondari wa Halmashauri ya Mji wa Babati Paskalina Lowokelo ambapo shule iliadhimisha mambo matatu makubwa katika siku hiyo.
Kwanza ilifanyika ibada ya shukurani Iliyongozwa na Mchungaji Kiongozi wa KKKT Usharika wa Mrara Baba Mchungaji Daniel Gishinde kama shukrani ya tasisi hiyo kwa Mungu kwa mambo mengi mema ambayo Mungu amekuwa akiwatendea kwa takribam Miaka 11 sasa tangu kuanzishwa kwa shule hiyo.
Pili walifanya mahafali ya darasa la saba ambapo wanafunzi 31 walikabidhiwa vyeti na zawadi mbalimbali zikiwemo za taaluma, michezo, uongozi, usafi na nidhamu.
Na pia Taasisi hiyo iliadhimisha siku ya Tarangire Day siku ambayo huwa inadhimishwa kila mwaka mwezi Septemba tangu kuanzishwa kwa shule hiyo Septemba 2016.
Ubunifu huu ndiyo uliopelekea Taasisi nyingi nchini kuanza kuadhimisha siku muhimu katika tasisi zao kama Simba Day na Yanga day miaka ya hivi karibuni.
Mgeni Rasmi katika mafali hiyo amewaasa wahitimu kuwa wasiwe na sura tofauti tofauti kwa nyakati tofauti bali wawe wanyenyekevu na watiifu.
“Unapokuwa Kanisani au Msikitini uwe na sura hiyo hiyo shuleni, nyumbani, shule ya msingi, sekondari, kidato cha Kwanza na hata cha pili na kuendelea,” amesema Paskalina.
Amesema katika kidato cha pili baadhi ya wanafunzi hubadilika sura zao na kuwa na sura tofauti na matendo mabaya hivyo akiwasa wanafunzi, wazazi na walimu kuwa makini sana katika kipindi hik kwani baadhi hupotea njia katika maisha.
Afisa mtendaji mkuu wa Shule CPA Ronald Moshi amesema shule ina azma zake ambazo ni juhudi katika taaluma (Effort in Accademics), hofu ya Mungu (Meditation) na usafi wa mwili, moyo, matendo na mazingira (Cleaness).
Kilichowavutia watu wengi katika mahafali hiyo ni mwanafunzi wa kabila la kimasai kutoka wlayani Chemba Mkoani Dodoma Kamando Matata Kisai ambae aliandikishwa shuleni hapo mwaka 2018 akiwa hafahamu kuongea kishwahili wala Kingereza.
Ila siku hiyo mtoto huyo aliongea kingereza cha Uingereza bila kusoma popote tena kwa kujenga hoja mbalimali.
Hii ikawa ni sambamba na dhumuni la shule hiyo la kuanzisha thamani endelevu kwa wadau wake wote wanafunzi, wazazi, walimu na jamii (To create a sustainable value).
Mkuu wa shule hiyo Eva Mrutu amesema shule yake ni shule ya pekee mjini Babati iliyojikita katika huduma ya utoaji wa elimu mkoani Manyara kwa ada nafuu ambapo mabasi yake huenda vijiji ambavyo havina huduma ya shule za mchepuo wa kingereza.
Amesema mabasi yao hufuata wanafunzi kutoka maeneo kama ya Dareda mission, Dareda Kati, Riroda, Mamire, Endakiso na Endanachan na kuwafiki shuleni.
Wapo pia wanafunzi wa bweni toka wilaya za Simanjiro, Kiteto, Hanang, Mbulu na wengine toka Mikoa ya Singida, Arusha, Dodoma na Kilimanjaro.

