Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza S. Johari Mgeni Rasmi uzinduzi wa Kamati ya Ushauri Ngazi ya Mkoa na Wilaya na Kliniki ya Sheria bila malipo kwa Wananchi wa Mkoa wa Arusha, tarehe 24 Novemba, 2026.
Uzinduzi huo utafuatiwa na utoaji wa huduma mbalimbali za Kisheria bila malipo kwa wananchi wa mkoa wa Arusha kwa muda wa siku saba hadi tarehe 29 Novemba, 2026 katika Viwanja vya Sanawari Mataa.
