Mkurugenzi wa kampuni hiyo ,CPA Cornely Kilatu akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha leo 

Na Happy Lazaro, Arusha.

Kampuni ya eAudit Next imewataka wakaguzi wa ndani kutumia mifumo ya kidijitali ambao ni wa kisasa zaidi wa ukaguzi wa ndani katika shughuli zao za ukaguzi ili kuongeza ufanisi, kupunguza gharama na kwenda sambamba na mabadiliko ya teknolojia katika taaluma ya ukaguzi.

Akizungumza wakati wa mkutano Mkuu wa Wakaguzi wa Ndani unaofanyika jijini Arusha, Mkurugenzi wa kampuni hiyo ,CPA Cornely Kilatu amesema kampuni hiyo imebuni mfumo mpana zaidi Africa (Governance ecosystem) unaowasaidia wakaguzi katika maeneo mbalimbali kufanya kazi kwa weledi na viwangu. Mfumo huu unajumuisha eAudit next kwa ajili ya wakaguzi wa ndani, eRisk Next kwa ajili usimamizi wa vihatarishi (risk management, eCompliance management, eFraud management, e-Governance pamoja na eAudit Analytics.

Amesema mfumo huo unamwezesha mkaguzi wa ndani kufanya kazi kwa haraka zaidi, huku ukidaiwa kupunguza muda wa ukaguzi kwa hadi asilimia 30, hali inayoweza kusaidia taasisi kukamilisha kazi za ukaguzi kwa muda mfupi ikilinganishwa na matumizi ya taratibu za kawaida.

Tayari taasisi nchini Tanzania wameanza kuchangamkia ubunifu huu.

“Kwa sasa mfumo huu unapunguza muda wa ukaguzi kwa asilimia 30. Kwa mfano Kazi ambayo inaweza kuchukua siku kumi, inaweza kukamilika kwa muda mfupi zaidi kwa kutumia mfumo huu,” amesema Kilatu.

Ameongeza kuwa matumizi ya teknolojia yanaweza pia kupunguza gharama za ukaguzi kwa kusaidia idara kufanya kazi kwa ufanisi bila kutegemea idadi kubwa ya wakaguzi. Mfumo huo unaweza kutumiwa na idara ndogo yenye mkaguzi mmoja au wawili, pamoja na taasisi zenye idara kubwa za ukaguzi.

CPA Kilatu amesema kuwa,mfumo huo tayari inahudumia taasisi mbalimbali zikiwemo benki, mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) Tanzania na Zanzibar pamoja na kampuni za biashara, huku kampuni hiyo pia ikitoa mafunzo kwa wakaguzi kuhusu matumizi ya mifumo hiyo bila gharama.

Amesema mafunzo hayo yanawalenga kuwawezesha wakaguzi kutumia teknolojia katika audit management, risk management, compliance management, fraud management na kufanya ukaguzi kwa njia ya kidijitali.

Aidha amesisitiza umuhimu wa wakaguzi kuachana na utegemezi mkubwa wa taratibu za kawaida za manual katika kipindi ambacho teknolojia inabadilisha kwa kasi taaluma hiyo.

Kilatu ameongeza kuwa,mfumo wa *eAudit Analytics* unasaidia kuchambua taarifa nyingi kwa haraka hadi billioni 1 ndani ya dakika chache, pia ikiweza kufanya sampling, ukokotozi (computation) na kadhalika,, jambo ambalo linaweza kuwa gumu endapo litafanywa kwa njia za kawaida.

Kampuni hiyo imeshiriki mkutano huo kama mdhamini na mwezeshaji kwa lengo la kuwaunganisha wakaguzi wa ndani na zana pamoja na teknolojia zinazoweza kusaidia kuongeza thamani katika ukaguzi wa kisasa.