Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Sheikh Ahmed bin Rashid Al Maktoum, ndugu wa Mheshimiwa Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu na Mtawala wa Dubai.

Kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Tanzania, Rais Dkt. Samia anatoa pole kwa Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum, Familia ya Kifalme ya Al Maktoum, Serikali na wananchi wa Umoja wa Falme za Kiarabu, na kuwaombea faraja wafiwa wote.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi, Amin.