Mkuu wa Mkoa wa Arusha,CPA Amos Makalla akizungumza na waandishi jijini Arusha leo

Na Happy Lazaro, Arusha

MKOA wa Arusha unatarajiwa kuwa mwenyeji wa Kongamano la Tano la Wiki ya Ufuatiliaji na Tathmini litakalofanyika kuanzia Septemba 22 hadi 26, 2026, likilenga kuwakutanisha viongozi na watendaji kutoka taasisi mbalimbali kujadili uzoefu, ubunifu na mbinu bora za ufuatiliaji, tathmini na kujifunza katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha,CPA Amos Makalla ameyasema hayo leo jijini Arusha wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo kongamano hilo litakalofanyika katika Hoteli ya Ngurdoto, Arusha,

CPA Makalla amesema kongamano hilo linatarajiwa kuwa na uzito mkubwa kutokana na ushiriki wa viongozi na wadau mbalimbali.

Ameongeza kuwa , kongamano hilo litakuwa jukwaa la kitaifa la kubadilishana uzoefu na kujadili namna ya kuimarisha mfumo wa utoaji wa maamuzi unaozingatia takwimu na ushahidi sahihi, pamoja na kuongeza uwajibikaji katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

CPA Makalla amesema kuwa , kaulimbiu ya kongamano hilo ni “Kutoka Ushahidi Hadi Vitendo”, ikiwa na msisitizo wa kuimarisha ufuatiliaji na tathmini kwa maendeleo endelevu ya wananchi.

Amesema msisitizo huo unaendana na hatua ya Serikali ya kuhakikisha mipango inayopangwa inaonekana katika utekelezaji na matokeo halisi kwa wananchi.

Amesisitiza kuwa ushahidi wa maendeleo unapaswa kuonekana kupitia huduma zinazotolewa kwa wananchi, ikiwemo ujenzi na upatikanaji wa huduma za afya, elimu na maji, pamoja na namna Serikali inavyosikiliza na kutatua kero za wananchi.

Aidha, amesema maoni ya wananchi kuhusu huduma wanazopata ni sehemu muhimu ya tathmini ya utendaji wa Serikali.

CPA Makalla amesema ufuatiliaji na tathmini si zoezi la kitaalamu pekee, bali ni msingi wa upangaji na utekelezaji wenye tija, kwa kuwa unaiwezesha Serikali kufuatilia maendeleo, kupima matokeo na kufanya marekebisho kwa wakati ili kufanikisha utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2050, Malengo ya Maendeleo Endelevu pamoja na ajenda za maendeleo za Umoja wa Afrika.

Ameongeza kuwa, jukwaa hilo pia litatoa nafasi kwa Serikali, washirika wa maendeleo, sekta binafsi, asasi za kiraia na wananchi kujadili maendeleo ya nchi na kutoa mrejesho kuhusu mafanikio pamoja na maeneo yanayohitaji maboresho.

Amesema mrejesho huo utasaidia Serikali kuendelea kuboresha utendaji na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na wanakuwa na imani na taasisi zao.

“Arusha iko tayari kuwapokea wageni na wadau wote, huku akiwataka waandishi wa habari kushiriki kikamilifu katika kutoa taarifa kuhusu kongamano hilo, mijadala yake na matokeo yake, akisisitiza kuwa ingawa linafanyika Arusha, masuala yatakayojadiliwa yana umuhimu kwa nchi nzima.”amesema CPA Makalla.

Makalla ameongeza kuwa,kongamano hilo litawakutanisha viongozi na watendaji wa Serikali, wataalamu, washirika wa maendeleo, sekta binafsi, asasi za kiraia na wadau wengine kujadili uzoefu, ubunifu na mbinu bora za ufuatiliaji na tathmini, akitumia fursa hiyo pia kuwakaribisha Arusha na kuwahakikishia amani, usalama na ukarimu wa wenyeji wa Mkoa wa Arusha.

Amesema kaulimbiu ya kongamano hilo ni “Kutoka Ushahidi hadi Vitendo”, inayosisitiza matumizi ya takwimu na ushahidi katika kuchukua hatua na kuboresha utekelezaji wa mipango ya maendeleo, akibainisha kwamba utekelezaji wake ni sehemu ya kutimiza maono ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuacha tabasamu kwa wananchi kupitia utoaji bora wa huduma na kwa wakati kwa Watanzania wote.

Kwa upande wake Afisa matumizi wa ofisi ya Waziri Mkuu ,sera,bunge,Uratibu na wenye ulemavu idara ya ufuatiliaji tathmini ya utendaji wa serikali ,Charltom Meena amesema kuwa kongamano hilo linatarajia kuwashirikisha takribani washiriki 1,500.

Amesema kuwa,mada mbalimbali zitatolewa ikiwemo mbinu za ukusanyaji wa takwimu na matumizi ya takwimu