

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Dkt. Qu Dongyu, katika Makao Makuu ya FAO, jijini Rome, Italia, leo Septemba 21, 2026. Dkt. Mwigulu anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano wa Kimataifa wa Kujadili Afya Moja na Mifumo ya Chakula na Kilimo (One Health), unaofanyika Septemba 21–23, 2026. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, akisaini kitabu cha wageni katika Makao Makuu ya FAO, jijini Rome, Italia, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa FAO, Dkt. Qu Dongyu, leo Septemba 21, 2026. Dkt. Mwigulu yupo Roma, Italia kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano wa Kimataifa wa Kujadili Afya Moja na Mifumo ya Chakula na Kilimo (One Health), unaofanyika Septemba 21–23, 2026. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa Kujadili Afya Moja na Mifumo ya Chakula na Kilimo (One Health) wakimsikiliza Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, alipohutubia mkutano huo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri wa Kilimo, Daniel Chongolo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Ngwaru Maghembe pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk, wakimsikiliza Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, alipohutubia mkutano huo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, akizungumza katika Mkutano wa Kimataifa wa Afya Moja na Mifumo ya Chakula na Kilimo (One Health), leo Septemba 21, 2026, katika Makao Makuu ya FAO, Rome, Italia. Dkt. Mwigulu amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika mkutano huo unaofanyika Septemba 21-23, 2026 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
