Hili ni hatua yenye thamani kubwa kimkakati kwa TRC, kwa sababu inaiweka SGR katika nafasi ya kuwa zaidi ya mfumo wa usafirina kuwa jukwaa la huduma kwa jamii, afya na uhamasishaji wa wananchi.
*Maana ya ushirikiano huu kwa TRC*
Moja, inaongeza thamani ya SGR kwa jamii, yaani
kutoa huduma za uchunguzi wa magonjwa ya moyo ndani ya treni kunafanya safari ya SGR kuwa na thamani ya ziada kwa abiria. TRC inaonyesha kwamba reli si tu inasafirisha watu kutoka sehemu moja kwenda nyingine, bali pia inaweza kuwa njia ya kufikisha huduma muhimu za kijamii kwa wananchi.
Pili, Inaonyesha TRC kama taasisi inayotekeleza CSR kwa vitendo kwani
Ushirikiano na Jakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI) unaweza kuimarisha utekelezaji wa dhana ya *Corporate Social Responsibility* ambapo badala ya CSR kuonekana kama misaada pekee, hatua hii inaonyesha CSR inayolenga kinga, elimu na uchunguzi wa afya.
Tatu, inaunganisha TRC na ajenda ya afya ya Taifa kwakuwa magonjwa ya moyo ni suala muhimu la afya ya umma. Kwa kushirikiana na taasisi maalumu kama JKCI, TRC inaonyesha utayari wa kutumia miundombinu na mtandao wake wa usafiri kusaidia kufikisha ujumbe wa afya kwa idadi kubwa ya wananchi.
Nne, Inaongeza uhusiano chanya kati ya TRC na abiria kwakuwa biria wanapopata huduma ambayo hawakutarajia wakati wa safari, uzoefu wao wa SGR unaweza kubadilika kutoka kuwa transport experience kwenda kuwa customer and community experience. Hii inaimarisha uhusiano wa TRC na wateja wake.
Tano, inaipa SGR nafasi kama jukwaa la kampeni za kitaifa, kwa maana kwamba treni zina uwezo wa kufikisha ujumbe kwa watu wengi kwa wakati mmoja. Kwa hiyo, tukio hili linaweza kuwa mfano wa jinsi SGR inavyoweza kutumika kwa kampeni za kitaifa kuhusu afya, usalama, mazingira, elimu na masuala mengine ya kijamii.
Saba, Inaongeza taswira ya TRC kama taasisi inayojali watu
Kwa upande wa mawasiliano ya taasisi, ujumbe muhimu si tu kwamba “TRC imeshirikiana na JKCI”, bali kwamba “TRC inaweka ustawi wa wananchi katika sehemu ya uzoefu wa safari.” Hii ni asset muhimu katika kujenga corporate reputation.
Saba, Inaweza kuimarisha ESG ya TRC Hatua hii inaingia vizuri katika kipengele cha Social cha ESG, yaani namna taasisi inavyogusa maisha na ustawi wa jamii na ni sehemu ya ushahidi wa TRC kuhusu mchango wake kwa jamii.
