Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Septemba 17, 2026 atafungua na kufunga Kongamano la Kitaifa la Wanamipango, linalofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC)

Kongamano hilo linalokutanisha zaidi ya wajumbe 1300 kutoka mikoa yote Tanzania lina kaulimbiu isemayo: _Kutekeleza Dira ya 2050: Kuimarisha upangaji Jumuishi : Utekelezaji na Matokeo_

Baadhi ya viongozi wanaoshiriki katika kongamano hilo ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Tausi Kida na Mjumpe wa Tume ya Taifa ya Mipango Balozi Ombeni Sefue.