Mbunge wa Jimbo la Namtumbo na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Juma Homera kulia,akikabidhi fedha Kiasi cha Shilingi milioni 5 kwa ajili ya akina Mama wa Kata ya Mchomoro ambazo zitawawezesha kuanzisha miradi ili kujikwamua kiuchumi.

Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Mingwea Kata ya Mchomoro Wilayani Namtumbo,wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Dkt Juma Homera

………..

Na Mwandishi Wetu, Namtumbo

WAZIRI wa Katiba na Sheria Dkt Juma Homera,amewataka watendaji wa Serikali wilayani Namtumbo kutimiza wajibu wao kwa kutatua kero na changamoto za wananchi badala ya kusubiri wafike viongozi wa ngazi ya juu na kufanya hivyo ni kushindwa kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan.

“Ni muhimu kwa watendaji Serikalini kuanzia ngazi za chini tujikite zaidi kutatua kero katika jamii tunazoziongoza,hawa wananchi wetu wanahitaji msaada wetu kwa sababu hawana sehemu ya kukimbilia,wakija kwenye ofisi zetu lazima tuwasikilize na kuwasaidia kutatua keto zap,nawaomba Sana watendaji wa ngazi zite tusisubiri hadi wanapofika viongozi wa juu jambo hili sio sawa hata kidogo”alisema Dkt Homera.

Homera alisema hayo jana,wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi na viongozi wa Serikali katika kijiji ha Mingwea kata ya Mchomoro Halmashauri ya wilaya Namtumbo wakati wa ziara ya siku nne wilayani Namtumbo.

Alisema,baadhi ya changamoto zilizopo kwenye vijiji hazijapatiwa ufumbuzi kwa muda mrefu licha ya kufikishwa kwa Viongozi ili kupata msaada,hata hivyo viongozi wameshindwa kuchukua hatua jambo linaloweza kusababisha wananchi kuichukua Serikali yao.

Homera amelazimika kutoa agizo hilo baada ya kupata malalamiko ya wananchi wa kijiji hicho waliochanga zaidi ya Sh.milioni 8 ili wapatiwe eneo kwa ajili ya shughuli za kilimo,lakini kwa muda mrefu sasa hawajapata majibu ya maombi yao.

Kwa mujibu wa Homera,tabia hiyo haikubali na dhahiri watendaji wa aina hiyo wameshindwa kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan katika majukumu ya kuwatumikia wananchi wanaohitaji kupata huduma bora ,badala ya kuishi kwa mateso hivyo kushindwa kujikita katika shughuli za maendeleo.

Katika hatua nyingine Waziri Homera,amewataka watendaji hao kutoka maofisini na kwenda vijijini na mitaani kusikiliza na kumaliza ya migogoro ikiwemo ya ardhi iliyopo katika kijamii kabla haijawa mikubwa,kutatua ,kusimamia miradi kama ujenzi wa shule na miundombinu mingine inayotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine.

Homera ambaye ni mbunge wa Jimbo la Namtumbo,ameiagiza idara ya ardhi kwenda kijiji cha Mingwea kukutana na viongozi na wananchi na kutoa majibu waliyofikia kuhusiana na maombi hayo badala ya kukaa kimya huku wananchi wakiwa na uhitaji mkubwa wa ardhi kwa ajili ya kuendelea na shughuli za kilimo.

Mkazi wa kijiji cha Mingwea Athuman Ponera,ameiomba Serikali kupitia Halmashauri ya wilaya Namtumbo iwasadie kutafuta mwekezaji katika jumuiya ya uhifadhi wanyamapori ya Mbalang’andu ambayo imesimama kufanya shughuli zake baada ya kukosa mwekezaji.

Alisema, jumuiya hiyo ina manufaa na mchango mkubwa kwa maendeleo ya kata ya Mchomoro na wilaya ya Namtumbo kwa ujumla,lakini baada kukosa mwekezaji haina mchango wowote katika jamii.

Naye Tamasha Ngwai,amelalamikia wanyapori na waharibifu hususani tembo na nguruwe kuvamia mashamba na kula mazao,hivyo kusababisha baadhi yao kukosa chakula cha familia ambapo ameiomba idara ya maliasili isaidie kudhibiti wanyama hao.