Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji Tanzania, Bw. Mlida Mshota, Septemba 13,2026 amefika Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, nyumbani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa ajili ya kumfariji na kumpa pole kufuatia msiba wa kuondokewa na mume wake, Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan.Mshota ametoa pole kwa Rais Samia pamoja na familia kufuatia msiba huo, huku akiwawakilisha wafugaji Tanzania katika kipindi hiki cha majonzi.

Maalim Hafidh Ameir Hassan alifariki dunia Septemba 7, 2026, katika Hospitali ya Mzena, Zanzibar.