Wekundu wa Msimbazi, , wameibuka na ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Mighty Wanderers ya Malawi katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa leo, Septemba 10, 2026, katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Mabao ya Simba yamefungwa na Clatous Chama dakika ya 7 na 33, Libasse Gueye akifunga dakika ya 26 na 69, Keletso Makgalwa dakika ya 88 pamoja na Morice Abraham dakika ya 90+3,  kwa upande wa Mighty Wanderers, bao lao la kufutia machozi lilifungwa dakika ya 44 kupitia mkwaju wa penalti.

Ushindi huo umeiwezesha Simba SC kusonga mbele kwa jumla ya mabao 7 -1, baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Malawi.