Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, amemshukuru Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, kwa uongozi, malezi na ushirikiano alioutoa katika kipindi cha zaidi ya miezi kumi walichofanya kazi pamoja katika Wizara ya Nishati.

Mhe. Salome ameyabainisha hayo leo Septemba 09,2026 wakati akizungumza waati wa kumuaga Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi mbaye awali alikuwa Waziri wa Nishati iliyofanyika katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.

Amesema katika kipindi cha uongozi wake amejifunza umuhimu wa upendo, kuthaminiana na kushirikiana katika kutekeleza majukumu ya Serikali, akieleza kuwa kupitia Mhe. Ndejembi ameweza kuwa moja ya Manaibu Waziri bora katika Bunge na Baraza la Mawaziri.

“Katika kipindi cha uongozi wako nimejifunza mambo matatu ikiwemo upendo na kuthaminiana na kuwa na mahusiano mazuri, kufanya kazi kwa ushirikiano pamoja na kuwa na uthubutu wa kufanya maamuzi kwa kuangalia maslahi ya Taifa bila kujali maslahi binafsi hivyo sisi kama familia ya Nishati tunaendelea kukuombea katika majukumu yako mapya uendelee kuwa na utii na hekima katika ufanyaji kazi wako”. Amesisitiza Mhe. Salome.

Amesema kupitia Uongozi wa Mhe Ndejembi viongozi na watendaji wa Wizara ya Nishati wataendelea kusimamia misingi iliyowekwa katika kuendeleza Sekta ya Nishati huku akisisitiza kukamilisha kwa wakati miradi ya maendeleo aliyoicha katika uongozi wake kipindi alichokua Waziri wa Nishati.

Sambamba na hilo, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kumuamini Mhe. Deogratius Ndejembi na kumpa nafasi ya kulitumikia Taifa katika ngazi za juu za uongozi, jambo lililoendelea kuimarisha uaminifu na imani kwa Wizara ya Nishati katika utekelezaji wa majukumu yake kwa maslahi ya Taifa.

Mhe. Salome ameongeza kuwa, pamoja na kuwa Mhe. Ndejembi umeondoka katika Wizara ya Nishati, tunaomba uendelee kuwa sehemu ya familia ya Wizara ya Nishati, uwe mlezi wetu na tutakapohitaji ushauri, tunaomba utupokee na kuwaongoza, napale tunapokosea utukosoe ili tuweze kujirekebisha na kuendelea kuijenga na kuiimarisha Sekta ya Nishati nchini.