Leo jijini Dodoma, Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mh. Marianne Young amekutana na Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde, kwa ajili ya mazungumzo kuhusu sekta ya madini nchini Tanzania na fursa za kuimarisha ushirikiano kati ya Uingereza na Tanzania.
Mkutano huo ulijadili kuhusu uwekezaji, uongezaji wa thamani, na kuhakikisha sekta hiyo inachangia katika ukuaji wa uchumi unaoshirikisha wote.

Tanzania na Uingereza zitaendelea kushirikiana katika maeneo yenye manufaa kwa pande zote mbili ili kudumisha ustawi wa mataifa yote mawili.
