Mkurugenzi wa shule ya mchepuo wa kiingereza ya Deanery Pre &primary ,Elibariki Nnko akizungumza katika mahafali ya sita ya darasa la saba ambapo jumla ya wanafunzi walihitimu.

Happy Lazaro,Arusha .

Arusha. WAZAZI wametakiwa kuacha kuwahukumu watoto kwa kusema hawana nidhamu bila kuanza kujiuliza kama wameweka sheria na taratibu zinazopaswa kufuatwa ndani ya familia.

Hayo yameelewa na Mkurugenzi wa shule ya mchepuo wa kiingereza ya Deanery Pre &primary ,Elibariki Nnko wakati akizungumza katika mahafali ya sita ya darasa la saba ambapo jumla ya wanafunzi walihitimu.

 Imeelezwa kuwa nidhamu ya mtoto huanza pale ambapo mzazi anaweka mipaka, sheria na taratibu za kumwelekeza mtoto katika maisha ya kila siku. 

“Mtoto anapokiuka taratibu hizo ndipo mzazi anapokuwa na msingi wa kusema mtoto hana nidhamu, lakini kama hakuna sheria zilizowekwa nyumbani, lawama haziwezi kuelekezwa kwa mtoto pekee.”amesema Nnko.

Aidha amesema kuwa , wazazi wameelezwa kuwa familia nyingi zimekuwa zikikabiliwa na changamoto ya malezi kwa sababu watoto wanaachwa kufanya mambo wanayotaka bila kuwekewa mipaka.

 “Baadaye wazazi huanza kulalamika kuwa watoto wameharibika au hawana nidhamu, wakati mwingine tatizo linatokana na kushindwa kwa wazazi kutekeleza wajibu wao wa msingi wa kuweka mfumo wa malezi. amesema Nnko.

“wazazi wanapaswa kujitambua kuwa wao ni viongozi wa familia na wanawajibika kuweka misingi itakayowaongoza watoto.”amesema .

Amesema kuwa, familia inaweza kulinganishwa na taasisi nyingine zinazoongozwa kwa sheria na taratibu.

 “Kama ambavyo nchi ina viongozi wanaosimamia sheria na taratibu ili kuhakikisha mambo yanaenda kwa utaratibu, vivyo hivyo baba na mama wanapaswa kushirikiana katika kuongoza familia, Sheria hizo hazipaswi kuwa za maneno pekee, bali wazazi wanapaswa kuhakikisha zinatekelezwa kwa uthabiti, busara na upendo ili watoto wajue mipaka yao na wajibu wao.

Wazazi pia wamehimizwa kuelewa kuwa malezi si jukumu la mzazi mmoja, bali ni wajibu wa familia kwa ujumla. 

Baba na mama wanapaswa kukubaliana kuhusu misingi ya malezi, namna ya kuwafundisha watoto na hatua zinazopaswa kuchukuliwa pale wanapokiuka taratibu. Ushirikiano huo utasaidia kuondoa mkanganyiko kwa watoto ambao wakati mwingine hupewa maelekezo tofauti na wazazi wao, jambo linaloweza kudhoofisha nidhamu na heshima ndani ya familia.

Aidha, imeelezwa kuwa malezi hayapaswi kuonekana kama jukumu linalomalizika mtoto anapofikisha umri wa utu uzima

 Hata mtoto anapokuwa na miaka 30 au zaidi, akiwa ameoa au kuolewa na kuanzisha familia yake, mzazi bado ana nafasi ya kumshauri na kumwelekeza.

 “Tofauti ni kwamba kadiri mtoto anavyokua, namna ya kumwelekeza inapaswa kubadilika kutoka kwenye kumwamrisha kama mtoto mdogo hadi kumshauri kwa hekima na heshima kama mtu mzima.”amesema 

Aidha ametumia.nafasi hiyo kuwaasa wazazi wameaswa kujenga uhusiano mzuri na watoto wao ili hata wanapokuwa watu wazima waweze kurudi nyumbani na kusikiliza ushauri wa wazazi wao. 

Mzazi anapaswa kuwa mtu wa kumjenga mtoto, kumwelekeza pale anapokosea na kumsaidia kufanya maamuzi sahihi, badala ya kusubiri mtoto afanye kosa ndipo aanze kulaumiwa. Malezi bora yanahitaji uvumilivu, mawasiliano na mfano mzuri kutoka kwa wazazi wenyewe.

“Familia inayoweka misingi mizuri tangu mwanzo huandaa watoto wenye uwezo wa kujiongoza hata wanapokuwa watu wazima. Kwa hiyo, badala ya kusema tu “watoto wa siku hizi hawana nidhamu,” wazazi wanapaswa kujiuliza wamefanya nini katika kuwajengea .”amesema

 

Kwa upande wake mgenirasmi katika.mahafali hayo Meneja wa benki ya Azania tawi la ABC ,Cythia Tarimo amewataka wahitimu kutambua kuwa elimu waliyoipata katika shule yao ni msingi wa safari yao ya maisha, huku wakihimizwa kuendelea kusoma kwa bidii, kuwa na nidhamu, kuheshimu wazazi na walimu pamoja na kuchagua marafiki watakaowasaidia kufikia malengo yao. 

Tarimo amewapongeza walimu na uongozi wa shule kwa jitihada wanazofanya katika kutoa elimu na malezi bora, akisema watoto wanaolelewa shuleni ni sehemu muhimu ya taifa la kesho.

 

Amesema elimu haipaswi kuishia kwenye ufaulu wa darasani pekee, bali inapaswa kuwajenga wanafunzi wenye maadili, ubunifu, kujiamini na uwezo wa kukabiliana na changamoto za maisha.

 

 

Aidha amewataka wazazi kuwafungulia watoto akaunti za benki na kuwajengea utamaduni wa kuweka akiba hata kwa kiasi kidogo, huku watoto wakifundishwa pia umuhimu wa kusaidia wengine na kupanga maisha yao ya baadaye.

 

 

Hata hivyo amewataka wahitimu hao kutokata tamaa wanapokutana na changamoto, bali kuwa na ndoto kubwa na kuzifanyia kazi kwa bidii kwani elimu inaweza kuwafungulia fursa za kiuchumi, kuongeza uwezo wa kujieleza na kujenga heshima katika jamii.

 

“Nawaomba mtambue umuhimu wa kumshirikisha Mungu katika maisha yenu na kutunza maadili mliyojengewa shuleni hata baada ya kuhitimu.”amesema .

 

 

Aidha amewataka wahitimu hao kuendelea kuwa na umoja na kuanzisha mtandao imara wa alumni utakaowawezesha kusaidiana katika maisha yao ya baadaye. 

 

Hata hivyo amewataka kutokuisahau shule yao baada ya kuondoka, bali kutumia umoja wao kuitangaza, kuiunga mkono na kushiriki katika maendeleo yake, wakikumbuka kuwa shule hiyo ndiyo iliyoweka msingi wa elimu na malezi yao.

 

“Naomba niweke msisitizo katika umuhimu wa kuwapatia watoto elimu ya fedha tangu wakiwa wadogo, ikiwemo kuwafundisha kuweka akiba, kutumia fedha kwa nidhamu na kuanza kujifunza kuhusu uwekezaji.”amesema 

 

Aidha ameipongeza shule hiyo kwa kuwapa wanafunzi fursa ya kuendeleza vipaji kupitia shughuli za ziada, ikiwemo sanaa na ngoma, huku ikihimizwa kuendelea kuwaongezea maarifa ya ujasiriamali na elimu ya fedha. 

 “Mchanganyiko wa elimu ya darasani, malezi, nidhamu, vipaji, ujasiriamali na maarifa ya fedha utawasaidia wahitimu kuwa watu wenye uwezo wa kujitegemea, kuajiri wengine na kutoa mchango chanya katika familia, jamii na Taifa”.amesema . Meneja wa benki ya Azania tawi la ABC ,Cythia Tarimo akizungumza katika mahafali hayo jijini Arusha