Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (kulia), akiagana na Waziri wa Fedha, Bajeti na Sekta ya Benki wa Comoro, Mheshimiwa Moussa Abderemane, wakati walipokutana na kufanya mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine walijadili umuhimu wa kuweka mazingira rafiki yatakayorahisisha usafirishaji wa bidhaa, huduma, mitaji na wafanyabiashara kati ya Tanzania na Comoro na kwamba hatua hiyo inaweza kusaidia kuongeza biashara, uwekezaji na ajira.

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (katikati upande wa kushoto) akiongoza kikao chake na ujumbe wa Serikali ya Comoro ukiongozwa na Waziri wa Fedha, Bajeti na Sekta ya Benki wa Comoro, Mheshimiwa Moussa Abderemane (Katikati upande wa kulia), wakati walipokutana na kufanya mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine walijadili umuhimu wa kuweka mazingira rafiki yatakayorahisisha usafirishaji wa bidhaa, huduma, mitaji na wafanyabiashara kati ya Tanzania na Comoro na kwamba hatua hiyo inaweza kusaidia kuongeza biashara, uwekezaji na ajira.

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akizungumza wakati wa kikao chake na ujumbe wa Serikali ya Comoro ukiongozwa na Waziri wa Fedha, Bajeti na Sekta ya Benki wa Comoro, Mheshimiwa Moussa Abderemane (Katikati upande wa kulia), wakati walipokutana na kufanya mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine walijadili umuhimu wa kuweka mazingira rafiki yatakayorahisisha usafirishaji wa bidhaa, huduma, mitaji na wafanyabiashara kati ya Tanzania na Comoro na kwamba hatua hiyo inaweza kusaidia kuongeza biashara, uwekezaji na ajira.

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (Katikati), Waziri wa Fedha, Bajeti na Sekta ya Benki wa Comoro, Mheshimiwa Moussa Abderemane (wanne kushoto), Balozi wa Comoro nchini Tanzania, Mhe. Dkt. Ahamada El Badaoui Mohamed (wa tatu kulia), wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kikao chao kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine kilijadili umuhimu wa kuweka mazingira rafiki yatakayorahisisha usafirishaji wa bidhaa, huduma, mitaji na wafanyabiashara kati ya Tanzania na Comoro na kwamba hatua hiyo inaweza kusaidia kuongeza biashara, uwekezaji na ajira. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar es Salaam)
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amesema kuwa Tanzania ina dhamira ya kuimarisha zaidi ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo na Serikali ya Jamhuri ya Comoro, ili kuleta manufaa ya pamoja kwa wananchi wa nchi hizo mbili.Mhe.
Alisema kuwa lengo la ziara yake nchini Tanzania, akiambatana na ujumbe wake, lilikuwa kujifunza namna Tanzania ilivyopiga hatua kubwa ya matumizi ya mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika ukusanyaji na usimamizi wa mapato ya Serikali.
Aliahidi kuwa watayatumia matokeo ya ziara yake hapa nchini kuboresha mifumo yao ya ukusanyaji mapato ya Serikali kwa kutumia TEHAMA na mifumo ya kodi hatua itakayochochea zaidi ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo.
Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Balozi wa Comoro nchini Tanzania,Mhe. Ahamada Elbadaoul Mohamed fakih, Mkurugenzi wa Masoko wa Kanda wa Kampuni ya SoftNet Technologies Bw. Maharage Chande, na viongozi wengine kutoka Tanzania na Comoro.
