Na Victor Masangu, Bagamoyo
 Baraza la michezo  la Taifa (BMT) limeipongeza kwa dhati Taasisi ya Shajar inayomiliki shule ya Baobab kwa kuweza mipango madhubutti katika kukuza sekta ya michezo mbali mbali kwa wanafunzi na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiana na sapoti ya hali na mali katika kuendeleza maono waliyonayo katika kukuza vijapi vya watoto hasa wakiwa mashuleni.    
Kauli hiyo imetolewa na Afisa michezo  mwandamizi wa  (BMT)  Charles Maguzu   wakati  wa sherehe za miaka 20 ya Baobab ambayo iliambatana na utoaji wa zawadi mbali mbali kwa washindi  walioweza kuibuka  kidedea katika michezo mbali mbali ikiwemo, mchezo wa soka, riadha, pete, pamoja na michezo mingine ambapo washindi walizawadiwa vikombe pamoja na medali.
Mwandamizi huyo amesema  kwamba wao kama serikali kupitia baraza hilo  wataendelea kushirikiana bega kwa bega na uongozi wa shule hiyo katika kukuza vipaji mbali mbali walivyonavyo wanafunzi wa shule hiyo kwani kwa lengo la kuweza kuwaendeleza zaidi kufika mbali.
Kadhalika Maguzu amewahiimiza walimu, na wazazi wanaendelea  kuhakikisha wanalinda  suala  la watoto wao  kuwa na malezi bora pamoja na kuwa wazalendo na nchi yao ikiwa pamoja na upendo ambao utawezza kuwafanya kufanya vizuri zaidi katika suala la elimu pamoja na mambo ya michezo mbali mbali.
“Kwa kweli nawapongeza kwa dhati uongozi mzima wa shule ya Baobab kwa kuwewza kunialika katika siku hii ambayo ni muhimu sana na kitu kingine niwapongeze kwa kuweka mikakakti madhubuti ya  kuwaendeleza wanafunzi wenu katika nyanja ya michezo sambamba na masomo hii ni hatua nzuri sana na sisis kama serikali  tutakuwa nanyi bega kwa bega katika kutimia malengo yenu”, Maguzu
 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Shajar Shani Swai ambayo ndiyo inayimiliki shule hiyo ya Baobab amebainisha kwamba wanaishukuru serikali kwa kuweza kuendelea kutoa sapoti ya hali na mali katika suala zima la kuboresha elimu pamoja na kushirikiana nao katika nyanja ya kukuza michezzo na vipaji kwa wanafunzi.

Maadhimisho ya  miakaa 20 ya Taasisi hiyo  ya Shajar yamekwenda sambamba na kufanyika kwa michezo mbali mbali pamoja na mbio za Marathon ambazo ziliandaliwa maalumu kwa ajiloi ya kuweza kuwasaidia watoto yatima na wenye mahitaji maalumu huku viongozi wa serikal viongozi wa dini, wakuu wa shule,taasisi wezeshi, wakuu wa Wilaya, wabunge pamoja na mawaziri walihudhulia kwa nyakati tofauti katika maadhimisho hayo.