Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo, ameondoka nchini Tanzania baada ya kukamilisha ziara yake ya kikazi ya siku mbili.
Mhe. Rais Tshisekedi, akiambatana na ujumbe wake, ameagwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Zanzibar, na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo, pamoja na viongozi wengine wa Serikali.
Ziara hiyo imeimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na DRC, hususan katika maeneo ya kidiplomasia, kiuchumi na kijamii, pamoja na kuweka msingi wa utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizo mbili.


